
Wapenda wetu na wadau wetu, kwanza kwa hesima na taadhima nianze kwa kuwasabahi; je hamjambo? bila shaka mu bukheri wa afya,
Awali ya yote nianze kwa kujitambulishe kwenu kuwa mimi naitwa Daniphord Anderson Mwajah, mwanzilishi na muasisi wa shirika lisilo la kiserikali liitwalo Twiga Vision Tanzania.
Shirika la Twiga Vision Tanzania limeanzishwa mahususi kabisa kutoa fursa kwa watu wasio na fursa ili kufikia malengo yao, mfano; asiye na elimu aipate elimu, asiye na kazi aipate kazi, na asiye na taarifa muhimu kuhusu mambo muhimu yanayomkabili naye pia apate hizo taarifa! Kwa upande wa makundi tunayoyalenga zaidi ni akina mama na vijana kwa ujumla wao.
Kazi zetu ni kuelimisha jamii juu ya njia mbalimbali za kufanikishwa malengo yao, sisi tunaamini kuwa kila binadamu ana nafasi na uwezo wa kufanikisha jambo na kwa sababu hiyo tunahamasisha watu kubuni na kutekeleza miradi ya kimaendeleo kwa ngazi ya mtu binafsi na kwa ngazi ya jamii kwa ujumla.
kwa maelezo zaidi tutembelee kwenye ukurasa wetu wa facebook:
https://www.facebook.com/TwigaVisionTanzania?ref=hl
Au tembelea Tuvuti yetu:
www.twigavisiontanzania.org